TAPHGO wameandaa mkutano na wadau mbalimbali kama CEDESOTA, PINGOs na wadau wengine wanaojihusisha na ufugaji asilia kujadili sheria namba 5 (1999) ya ardhi ya vijiji. Mkutano huo umefanyika tarehe 1 / 7/ 2015 Equator Hotel, Arusha. Lengo la ufugaji asilia ni kuongeza pato la taifa na kukidhi maisha ya wafugaji.
Kulingana na sheria ya ardhi iliopo kuna baadhi ya vipengele ambavyo wadau hao wameona vinahitaji marekebisho na maboresho kwa sababu vina mapungufu. Pia kuna zingine za kuongeza ivo wameandaa hoja za msingi na kwa pamoja wamechambua na watawasilisha kwa serikali kwa ajili ya mapitio ili iweze kusaidia kwenye kuboresha sheria ya ardhi.
Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na kujadiliwa ni pamoja na;
- Migogoro sugu husababishwa na halmashauri kutopimwa, siasa zinazosababisha kuwatenga watendaji n.k
- Kutoheshimu haki za watu wachache (minority rights)
- Kutoheshimu rasilimali za wafugaji, wakulima, wavuvi, wachimbaji n.k
Kufuatia sababu zilizotajwa hapo juu, wadau au asasi hizi zimekuwa ndiyo chombo cha ushawishi kikiwasilisha mchango wa kila asasi ili kufikia lengo maalum ambalo ni kutetea haki za wafugaji asili.